VIDEO Queen asiyeishiwa na vituko Bongo, Lulu Diva amefunguka kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya mastaa kupora mabwana wa wenzao ila kwa atakayemfanyia mchezo huo atalipiza bila kujali lolote.
Lulu alifunguka hayo baada ya kutuhumiwa
kunyakua mpenzi wa dada mmoja aliyefahamika kwa jina la Grace ambapo
inadaiwa kajimilikisha mwanaume huyo wakati akijua ndiye anayemuweka
mjini shosti wake huyo.
“Yaani Lulu hana hata aibu, kuna dada
mmoja ni rafiki yake, anaitwa Grace. Yule dada alikuwa na jamaa yake
anayemuweka mjini, cha ajabu Lulu sijui wamekutana wapi na mwanaume
huyo, kamchukua na sasa yuko naye,” kilidai chanzo hicho kilichoomba
hifadhi ya jina lake.
Baada ya kupata ubuyu huo, mwandishi
wetu alimtafuta Lulu alipopatikana alisema kwa shari: “Kinamuuma ee,
yeye aliponichukulia wangu alidhani nimefurahi? Sasa kwa taarifa tu ni
kwamba mimi anayenipora bwana wangu, siku wake akinikalia vizuri
nalipiza.”
CHANZO; GPL

0 comments:
Post a Comment