Msanii
wa muziki wa bongo fleva Msami ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo
wake mpya 'Mabawa' amefunguka na kusema ni kweli alikuwa anatoka
kimapenzi na Irene Uwoya lakini toka wameachana wamebaki kuwa marafiki
na hawana tatizo lolote lile.
Msanii
akiwa kwenye kipindi cha Planet bongo kinachorushwa na EATV amedai kuwa
hata alipokuwa akitoka na Irene alikuwa hana tabia ya kumfuatilia
katika mambo yake ayafanyayo ila adai licha ya kuwa mahusiano yao
yalikufa lakini wamekuwa wakiwasiliana kama kawaida.
"Ndiyo
ni kweli nilikuwa natoka na Irene Uwoya lakini katika kipindi chote
hicho sikuwahi kumfuatilia katika mambo yake alikuwa huru kabisa, japo
tumeachana lakini mimi na yeye tupo sawa kabisa kwani mawasiliano yapo
kati yetu" alisema Msami.
Pia
msanii huyo amedai kuwa yeye aliamua kujiweka tofauti na baadhi ya
'Dancers' ambao wanafanya kazi na wasanii mbalimbali ili tu akuze
thamani yake katika kazi yake hiyo.
"Unajua
mimi nilifanya kwa muda kuwa chini ya msanii fulani lakini nikaamua
kujiweka tofauti ili niweze kujiongeza thamani yangu, kama hivi msanii
yoyote ambaye atahitaji mimi kumsaidia jambo fulani kuhusiana na kazi
yangu ya kucheza anakuwa anatambua thamani yangu katika jambo hilo"
alisema Msami.
0 comments:
Post a Comment