Wednesday, August 3, 2016

thea
Msanii wa filamu, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka kwa kusema kuwa bado ana mpango wa kuingia bungeni katika uchaguzi ujao wa 2020.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Thea amesema ndani ya kipindi hiki anaanza kujipanga zaidi kwa ajili ya uchaguzi ujao.
“Nimeona kuna kitu ndani yangu, yaani nataka kuongoza sema mwaka jana sikujipanga vizuri lakini uchaguzi ujao (2020) nitaingia kwa miguu miwili,” alisema Thea.
Muigizaji huyo amesema uchaguzi uliyopita aliutimia kama funzo katika maisha yake mapya ya uanasiasa.
Pia alisema tayari ameshajipima na kuona anaweza kufanya kitu kikubwa kwa wananchi kama akipata nafasi ya kuingia bungeni.

0 comments:

Post a Comment