Posted by Williammalecela.com on Friday, August 19, 2016
Bingwa wa mbio za
mita 3000 kuruka viunzi na maji kutoka Kenya Ezekiel Kemboi
amenyang'anywa medali yake ya shaba aliyoishinda mjini Rio de Janeiro,
Brazil.
Kemboi, 34, aliyemaliza wa tatu katika mbio hizo, alikuwa amepewa nishani ya shaba. Lakini
Ufaransa ilikataa rufaa baada ya kubainika kwamba mwanariadha huyo
wakati mmoja, baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari
wakati akishiriki mbio hizo Jumatano. Mfaransa Mahiedine Mekhissi, aliyemaliza nafasi ya nne, amepandishwa hadi nafasi ya tatu na kupewa nishani ya shaba. Kemboi,
aliyeshinda Olimpiki za London 2012 katika michezo ambayo Mahiedine
Mekhissi-Benabbad alishinda fedha, tayari ametangaza kwamba atastaafu. Mshindi
wa mbio hizo za Rio alikuwa Mkenya Conseslus Kipruto ambaye pia aliweka
rekodi mpya ya Olimpiki , muda wake ukiwa 8:03.28.
Mmarekani Evan Jager alimaliza wa pili muda wake ukiwa 8:04.28. Muda wa Kemboi ulikuwa 8:08.47 na wa Mekhissi 8:11.52.
0 comments:
Post a Comment