MWANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR
ES SALAAM: Mara tu baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangallah kumpa saa 24 mmiliki wa
iliyokuwa Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan, Tabibu Juma Mwaka ‘Dk.
Mwaka’, Jeshi la Polisi linadaiwa kumfungia kazi kwa msako mkali wa
kumkamata.
Ijumaa
iliyopita, Waziri Kigwangallah alifika kwenye kliniki hiyo iliyopo
Ilala- Bungoni jijini Dar na kuliagiza Jeshi la Polisi kumsaka na
kumkamata Dk Mwaka kisha kumfikisha mahakamani mara moja kwa kukiuka
taratibu za kitabibu za tiba asilia licha ya kufungiwa lakini amekuwa
akiendelea kutoa huduma hiyo.
Habari
kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilieleza kuwa askari wa jeshi hilo
Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, wikiendi iliyopita waliendesha msako mkali wa
kumkamata Dk. Mwaka huku wakiweka ulinzi kwenye kliniki hiyo ili endapo
angefika wamkamate.
“Baadaye
askari waligawanyika, wapo waliokwenda nyumbani kwake (Mbezi- Beach)
lakini hawakumkuta hivyo wakaweka doria maeneo hayo ili akifika tu
wamkamate.
“Mbali
na huko, pia askari walipita kwenye viwanja vyake anavyopenda kujirusha
wikiendi hasa kwenye klabu moja maarufu iliyopo Mikocheni (Dar) bila
mafanikio.
“Pia waliweka ‘patroo’ kwenye uwanja wa ndege (JKIA) ili asipite kwenda nje ya nchi,” alisema mtoa habari wetu.
Akizungumza na Wikienda muda
mfupi kabla ya kwenda mitamboni juzi (Jumamosi) juu ya msako huo wa Dk.
Mwaka, Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani
alisema kuwa ni kweli polisi walikuwa wakimsaka jamaa huyo maeneo
tofauti ikiwemo nyumbani kwake.
“Kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa za mahali alipo Juma Mwaka atujulishe ili tumkamate mwenyewe,” alisema Kamishna huyo.
Tukio
la kufungiwa kwa Dk. Mwaka siyo la kwanza kwani alishafungiwa mara
mbili lakini baada ya muda aliendelea kutoa huduma kama kawaida hivyo
kuibua mjadala mzito.
0 comments:
Post a Comment