
Usiku
wa August 18 mtanzania Mbwana Samatta amefanikiwa kufunga bao kwa mara
nyingine kwenye michuano ya UEFA Europa Leagua wakati klabu ya ya KRC
Genk ikicheza dhidi ya Locomotiva Zagreb ya Croatia kuwania kupangwa
kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Samatta
alifunga bao dakika ya 47 likiwa ni bao la pili kwenye mchezo huo, bao
la kwanza la Genk lilifungwa na Leon Bailey kwa mkwaju wa penati na
kuipa klabu hiyo ya Ubelgiji uongozi wa bao 2-0.
Lakini
wenyeji walikuja juu na kusawazisha magoli yote na kushuhudia mchezo
huo ukimalizika kwa sare ya magoli 2-2. Magoli ya Locomotiva yalifungwa
na Mirko Marić kwa penati dakika ya 52 na dakika ya 59 Ivan Fiolić
akaisawazisha Locomotiva.
Dakika saba kabla ya mchezo kumalizika Samatta alipumzishwa nafasi yake ikachukuliwa na Karelis.
Mchezo
wa marudiano utapigwa August 25 huku safari hii Genk wakiwa kwenye
dimba lao la nyumbani Cristal Arena kuwaalika Locomotiva Zagreb kwenye
mchezo ambao Genk watakuwa wakihitaji ushindi, sare ya 0-0 au 1-1 ili
kusonga mbele moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment