Shamsa Ford
Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO
KUFUATIA
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumfungia Nay wa Mitego kufanya
muziki kutokana na nyimbo zake kukiuka maadili, mpenzi wake wa zamani,
Shamsa Ford amempa makavu na kumtaka aache kuimba matusi.
Akipiga stori na Za Motomoto News, Shamsa
alisema Nay wa Mitego ni baba mwenye watoto wanaomtegemea, anamuonea
huruma lakini ni lazima ajifunze kwa kuacha kuimba nyimbo za matusi,
badala yake aimbe za kueli-misha jamii.
“Namu-onea
huruma lakini anatakiwa kujifunza kuimba vitu vya kuelimisha jamii,
aachane na matusi kwani kila wimbo anaotoa mara nyingi huwa na maneno
makali,” alisema Shamsa.
0 comments:
Post a Comment