Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amemtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Hassan Abbas anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Hassan Abbas akieleza mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano.
Abbas alisema ameimepokea nafasi hiyo na yupo tayari kuanza kazi.
“Nimeshaandika na kulipwa kwa habari, nimeshakuwa mwajiriwa, nimeshakuwa mhariri wa gazeti la Jumapili, nimeshakuwa mhariri msaidizi na nikawa tena mhariri mkuu kwahiyo mnaweza kuona ni jinsi gani nimekaa katika kazi kwa kipindi kisichopungua miaka tisa, niwaombe tushirikiane,” alisema Abbas.
0 comments:
Post a Comment