Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na
video yake ya wimbo ‘Bayoyo’ ameiambia Bongo5 kuwa kauli hiyo ilimfanya
aonekane msaliti.
“AliKiba alijisikia vibaya kwa sababu alijua kama
ndo vile tena ndugu yake nimekuwa msaliti kumbe ni watu walipata
definition nyingine na ni kitu ambacho hakiwezekani ila niliweza kufanya
interviews nikaweka mambo sawa,” alisema Abdul Kiba.Akifafanua kauli
yake aliyozungumza na kutafsiriwa vibaya Abdul Kiba alisema “Siku ambayo
nilifanya interview walinielewa vibaya maongezi yangu, unajua
unaposikia kwamba kuna kazi hakuna kazi ya bure, kazi yoyote lazima iwe
na malipo, nilikubali kwamba kama WCB watanihitaji kwa kolabo au show
naweza nikajoin nao kufanya kazi ila sikutoa kauli kwamba naweza kwenda
label yao kwa sababu hata mimi na label yangu,”
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa team Kiba kwa kuendelea kuwasapoti wasanii wake pamoja na kazi zao.
0 comments:
Post a Comment