Msanii wa muziki wa Kizazi kipya ambae pia ni mmiliki wa studio za High Table Sound, Barnaba Classic.
Barnaba amefunguka na kudai kuwa video nyingi za Bongo flava zinashindwa kupenya kimataifa kwa sababu ya Audio mbovu.
Akiongea
kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Barnaba amedai sababu
kubwa hasa ni wasanii kuwekeza zaidi kwenye Video na kusahau matayarisho
mazuri ya Audio.
“Niwaombe
tu wasanii wenzangu, hatuwezi kutoboa kama tuna Audio Mbovu, lazima
tuwekeze pia kwenye audio, tunao maproducer wengi wazuri wa kufanya
Mastering”.“Tuwatumie hawa maproducer, mi nashangaa sana video
tunatayarisha kwa dola elfu 10 wakati Audio tunatumia dola elfu moja
pekee” Alisema.
0 comments:
Post a Comment