Hakuna
asiyejua aina ya muziki anaoufanya Nay wa Mitego. Ni muziki flani hivi
ambao huwa unaongea na wale ambao Nay anawaona kuwa wameenda wrong. Na
hivyo Nay wa Mitego huwa anawachana kupitia nyimbo zake.
Wapo
wakerekwa wengi wa nyimbo za mkali huyo, na pia mara kibao tumesikia
zikimletea matatizo hadi kufikia hatua ya kuvunjiwa kioo cha gari na
vitu kama hivyo. Na ndio sababu ya wasanii wengi wakubwa kuogopa kufanya
collabo na mkali huyo kwa kuogopa kuonekana mshiriki kwenye ngoma
ambayo imemzungumzia mtu fulani vibaya.
Imetokea mara kibao kwa
chorus killer Belle 9 kupigiwa simu na msanii Nay wa Mitego kutaka
kushirikishwa katika nyimbo zake lakini Belle 9 amekuwa akimkimbia Nay
kila mara.
Sasa leo wote wawili wamekutana na kipaza cha Pe na kila mmoja anafunguka yakwake kuhusiana na issue hiyo.
“Nay
wa Mitego kwenye ngoma zake anavyo wachanaga watu yani huwa ni moja kwa
moja anamaanisha yan. ndio maana mimi huwa namkimbia ili kuepuka
lawama.” Ni baadhi ya maneno ya Belle 9, huku Nay wa Mitego akidai kuwa
hawezi kumlaumu kwasababu yeye mwenyewe anajua aina ya muziki ambao
anaufanya.
0 comments:
Post a Comment