
MWISHONI mwa wiki iliyopita (juzi Ijumaa usiku) ilifanyika pati ya
kusherehekea kuzaliwa kwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ambayo imeibua mabifu upya. Pati hiyo
iliyohudhuriwa na mastaa wachache kutoka Bongo ambao ni pamoja na Moze
Iyobo, Aunt Ezekiel na wengineo ilifanyika Zanzibar ambapo licha ya
kufana, imeibua mtifuano upya kati ya Zari na wifi yake, Esma
Abdulkadiri na Diamond na mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga.
IVAN NA DIAMOND
Bifu
la wawili hawa lilikuwa limezimika, lakini lilirudi upya baada ya
juzikati Diamond kumzawadia Zari nyumba iliyopo Afrika Kusini kisha
kumrushia Ivan dongo kwa kuandika mtandaoni: “Wanakazana kujisifu
matajiri ilhali watoto wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga… halafu leo
yuleyule wanayemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa maskini, kajawa na
shida, kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora
kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda
sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South
Africa.”

NI DONGO KWA IVAN
Ujumbe huo moja kwa moja u l i o n e k a n a
kumhusu Ivan ambaye kipindi cha nyuma kwa kushirikiana na mshikaji wake
aliyefahamika kwa jina la King Laurence, walikuwa wakimtusi wakimsema
kuwa ni maskini ila wao wana pesa licha ya madai kuwa, nyumba wanayoishi
watoto wa Zari kule Sauzi ni ya kupanga. Baada ya dongo hilo, hali
ilichafuka huku Ivan akimrushia madongo Diamond sambamba kumtaka Zari
amwambie bwana wake (Diamond) aondoe ujumbe huo mtandaoni kwani hata
wanaye wakiuona wataumia. Inadaiwa kuwa, licha ya Ivan kuomba hivyo,
Zari alimjibu kuwa Diamond amegoma kwa maelezo kwamba, wao (King
Laurence na Ivan) ndiyo walioanza kumtusi.
ESMA NA ZARI
Bifu
lao lilihusishwa baada ya Esma kuulizwa sababu za kutomuwish wifi yake
katika siku yake ya kuzaliwa, kuonesha ‘analo na limemfika hapa’
alifunguka: “Siwezi kumuwishi, mbona Taraj (mwanaye) hakumuwishi wakati
ndiye aliyekuwa akicheza na mwanaye (Tiffah) nyumbani? Wee ukosane na
mimi umkasirikie hadi mtoto, ujinga huo. Siwezi kumuwishi Mbona Bi.
Snura (mama wa Diamond) alimuwishi akamfuta na mafumbo juu, akasababisha
watu wakamchamba!..... (anataja jina la mwandishi) nimekaa tumboni kwa
mama yangu miezi 9 ‘so’ mtu anavyomletea dharau siwezi kumpenda. Mbona
wote tumekaa nao vizuri haijawahi tokea haya mambo, kwa nini yeye?”
alihoji Esma.
FAMILIA YA DIAMOND YASUSA BETHIDEI Katika kile kinachoonesha kuna kitu
kizito nyuma ya pazia kati ya Zari na ndugu wa Diamond, inadaiwa hakuna hata mmoja aliyefika hali iliyoibua maswali mengi.
DIAMOND, ZARI VIPI?
Kufuatia
kuibuka kwa mabifu hayo sambamba na figisu nyingine, gazeti hili
lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Zari kupitia simu zao za
mkononi ili waseme lolote, lakini simu zao hazikuweza kupatikana.
0 comments:
Post a Comment