Posted by Williammalecela.com on Tuesday, September 27, 2016
Vikundi vya wafuasi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wamekusanyika katika Ofisi za CUF Makao
Makuu, Buguruni, Jijini Dar es Salaam wakisubiri kumpokea na kumuingiza
ofisini.
Wanachama hao wanadai ya kuwa wana barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa
inayomtambua Lipumba aliyetangaza kujiuzulu nafasi hiyo mwaka jana kama
Mwenyekiti halali wa CUF.
Kwa mujibu wa shuhuda eneo la tukio, inadaiwa kuwa geti la ofisi za
chama hicho limefungwa kwa ndani ambapo hakuna kiongozi yeyote aliyepo
ndani.
Wafuasi hao wa Lipumba wamesikika wakiimba na kucheza huku wakidai kuwa
wanasubiri msafara wa Lipumba ambao upo njiani kuelekea Makao Makuu ya
CUF hapo Buguruni.
Awali hapo jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro
alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenea katika mitandao ya jamii kuwa
Msajili wa Vyama vya Siasa ametoa barua inayoagiza Profesa Lipumba arudi
katika nyadhifa yake ya Uenyekiti na kuwataka wanachama wa CUF wasubiri
taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wao.
Hatahivyo, leo alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo alikiri CUF kupokea
barua kutoka kwa Msajili na kudai bado hawajaisoma ili kujua maudhui
yaliyomo ndani.
Ameongeza kuwa pamoja na hayo Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya
kuingilia maamuzi ya vikao vya chama chochote cha siasa.
0 comments:
Post a Comment