Siku
chache zilizopita mwanadada Linah Sanga alichafua hali ya hewa katika
mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kuawa anapost picha/video za
Idris Sultan huku akiambatanisha na caption zenye utata ukizingatia
Idris alikuwa ni mpenzi wa mwanadada Wema Sepetu.Moja kati ya caption za
Linah ambazo zilizua gumzo sana mtandaoni ni ile aliyoandika “Mungu
alituumba sote Why na sisi tusipendane???” huku akiwa ametupia na picha
ya Idris kitu ambacho
kiliipelekea post hiyo kupata comments zaidi ya
elfu moja (1,000).Mengi yalizungumziwa baada ya sakata hilo ikiwemo na
kuwa mwanadada Linah kwa sasa anatoka kimapenzi na Idris. Kama umekuwa
ukifuatilia post za Linah utagundua kuwa mwanadada huyo alikuwa akipokea
kichambo sio cha kitoto kutoka kwa mashabiki wa Wema Sepetu ukizingatia
mwanadada Wemani mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi mkubwa sana
barani Afrika.Ikiwa bado hilo la Idris linaelea elea Linah ameamua kuja
na jingine tena la kupost picha akiwa na mwanaume ambaye hamuonyeshi
sura yake kamili. Ni mengi yanaongelewa katika mtandao huo na moja kati
ya post hizo ni hii hapa.
Siku hizi imekuwa kama imezoeleka hivi kwa
baadhi ya wasanii pindi watakapo kufanya yao huwa wanakuja kama na kiki
hivi ili kujitengenezea mazingira flani kwa muda huo waweze kuzungumziwa
kwa malengo ya mipango yao iweze kupenya. Sina uhakika sana kuwa kwa
mwanadada Linah na hii pia ni kiki au la.
0 comments:
Post a Comment