Idadi
ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada
wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,
Erasto Msuya maarufu bilionea Msuya, imeongezeka na kufikia wawili baada
ya mwingine kuunganishwa nayo.
Awali,
Agosti 23, mwaka huu mshtakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa
bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.Hata
hivyo, juma moja baadaye, mfanyabiashara wa jijini Arusha, Revocatus
Evarist (40), alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo na
kuuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.
Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.
Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo.
0 comments:
Post a Comment