Kanichambua kama karanga mama. Chambua kama karangaaa
Good
morning mabibi na mabwana. Inatia moyo sana kuona msanii kutoka bongo
land anaweka rekodi na kuivunja mwenyewe. Mpaka sasa hakuna msanii
yeyote barani afrika ambaye Video zake zinatizamwa na watu wengi ndani
ya muda mfupi kama Mondi Platnumz.Sio kuwa tunajivunia Viewers ila
tunajivunia Mziki wetu kutoboa zaidi Anga za kimataifa.
Japo kuna
watu wachache walioanza kuleta chokochoko na kutaka wimbo huu mpya
ufungiwe kwa madai ya kutokuwa na maadili ila wengi wetu tunampongeza
kwa ubunifu na kumsaidia Bi Saida karoli kurudi tena masikioni mwa watu.
Binafsi baada ya kusikia wimbo huu niliamua Kudownload na wimbo wa
Saida karoli ili nione kama ameutendea haki wimbo huo.
Hongera Diamond platnumz na tunatarajia leo Tutahit 1M viewers ikiwa ni siku ya pili baada ya Salome Kufufuliwa.

0 comments:
Post a Comment