MAKUBWA!
Licha ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford kufunga ndoa
na mfanyabiashara maarufu Bongo, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, aliyekuwa
mpenzi wa mwanadada huyo Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’ ameibuka na kusema bado penzi lake na mrembo huyo litaendelea
kama kawa, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukudondoshea.
ALIANZA
KWA KUKACHA HARUSI Katika harusi ya Shamsa iliyofanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita msanii huyo hakuhudhuria kabisa jambo ambalo
lilisababisha gumzo kwa baadhi ya waalikwa wakiwemo wasanii wakidai
kwamba ameogopa na kuona aibu kwani alishindwa kufikia hatua hiyo ya
ndoa hivyo angeweza kupandwa na hasira na kufanya fujo. “Unajua nimekuja
kwenye hii harusi ili nimuone tu Nay wa Mitego atakuwa katika sura ya
aina gani maana huyu Shamsa alikuwa mpenzi wake na hakuweza kufikia
hatua ya ndoa wakati mwanamama huyu ni wife material na anajitambua.
“Lakini nimemtafuta simuoni kabisa inawezekana ameona aibu au ameepusha
shari kwani yule alivyo na hasira angeweza kufanya fujo hapa,” alisikika
msanii mmoja akijadiliana na mwenzake.
NAY
ASAKWA Baada ya kutoonekana kwenye harusi hiyo na watu kuzua gumzo,
gazeti hili lilimtafuta Nay wa Mitego ambaye alieleza kwamba
hakuhudhuria sherehe hiyo kwa sababu hakualikwa pia hakuwepo Dar kabla
ya kufunguka kilichopo mayoni mwake. “Shamsa hakunialika kwenye sherehe
yake hivyo nisingeweza kwenda pia sikuwepo Dar nilikuwa mkoani, amefanya
jambo jema kuolewa siyo mbaya,” alisema Nay wa Mitego.
AFUNGUKA
MAKUBALIANO YAO Mwanahabari wetu alipozidi kumchimba Nay kuhusu penzi
lake na Shamsa na maumivu atakayoyapata baada ya mrembo huyo kumilikiwa
na Chid Mapenzi, mkali huyo aliyezoeleka kwa kufunguka maneno ya shombo
kwa wasanii wenzake, alilisema: “Siku chache kabla ya kufunga ndoa
Shamsa alinifuata na kuniambia amepata mwanaume ambaye yupo tayari
kumuoa nami nikamwambia sawa aolewe maana ni jambo zuri.
PENZI
PALEPALE “Kuolewa siyo tatizo na siyo kwamba ndiyo mambo mengine
hayataendelea, nasema bado tunapendana sana na ndoa haizuii kitu
chochote. Mambo mengine yataendelea kama kawaida.”
ALICHOANDIKA
MTANDAONI Muda mchache baada ya ndoa ya Shamsa kufungwa, Nay aliandika
maneno haya katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram;
“Tangazo tangazo nasikia my cousin kaolewaaaa sasa huyo aliyemuoa ipo
siku nitampiga tukio kama hiiii nina hasira.”
SHAMSA
ANASEMAJE? Baada ya kusikia maneno ya Nay wa Mitego, Risasi
Mchanganyiko lilimgeukia Shamsa na kumweleza ambapo alikuwa na haya ya
kusema: “Ninachoweza kusema ni kwamba, ninampenda sana mume wangu na
ninamthamini sana, sitegemei kumsaliti wala kuachana naye mpaka Mungu
atakapotutenganisha.”
WOLPER
KUTOHUDHURIA Kuhusu tetesi za Jacqueline Wolper kushindwa kuhudhuria
kwenye sherehe hiyo kwa kile kilichodaiwa Chid Mapenzi aliwahi kuwa
mpenzi wake, Shamsa alisema; “Kiukweli sijui labda alikuwa na dharura
kama ilivyokuwa kwa Wema ambaye alinipa udhuru hivyo kuhusu kuwa mpenzi
wa mume wangu sijui maana namuona mume wangu ni mpya kabisa hajawahi
kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine yeyote.
”
TUJIKUMBUSHE Nay na Shamsa walipamba vyombo vya habari kwa muda mfupi
mwishoni mwa mwaka jana kisha wakamwagana na kuueleza umma kuwa wao
watabaki kuwa marafiki wa karibu.

0 comments:
Post a Comment