BENKI ya NMB imeendelea kutoa elimu kwa viongozi wa Halmashauri, Manispaa,Majiji na wananchi wa kada mbalimbali juu ya huduma za kibenki ambazo wamekuwa wakizitoa kupitia mkutano mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawalana Serikali za Mitaa(ALAT) unaofanyika kitaifa mjini Musoma mkoani Mara ambapo wajumbe zaidi ya 500 wanahudhuria mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene akisalimiana na meneja wa NMB tawi la Musoma, Sebastian Kayanga alipokuwa anaingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwembeni Complex kwaajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa mwaka wa ALAT Taifa. NMB imedhamini mkutano wa ALAT
Taifa kwa shilingi Milioni 206 ikiwa ni gharama za mkutano na zawadi kwaajili ya Meya bora waMwaka. Picha ni kulia ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Amos Mubusi.
Taifa kwa shilingi Milioni 206 ikiwa ni gharama za mkutano na zawadi kwaajili ya Meya bora waMwaka. Picha ni kulia ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Amos Mubusi.
Kupitia mkutano huo NMB imeelezea jinsi ilivyounganisha mfumo wake wa kibenki na mfumo waserikali za mitaa (LGRCIS) kufanikisha ukusanyaji mapato ya kwa wakati na bila kupotea na kuandaa vituo vya makusanyo ya fedha kusaidia serikali katika makusanyo.Akitoa mada kwenye mkutano huo ulioingia siku ya 2 hii leo,Afisa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa (NMB) Augustino Mbogella,amesema licha ya kusaidia serikali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato,benki hiyo pia imesaidia miradi ya maendeleo ya jamii ikilenga zaidi katika utoaji wa misaada katika sekta ya elimu na afya.
Waziri waNchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) George Simbachawene ,akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la NMB kwenye maonyesho ya ALAT
Wakati huo, viongozi na wananchi wameombwa kutembelea banda la NMB ilikuweza kupata elimu zaidi likiwemo pia suala la ufunguaji wa akaunti mbalimbali kwenye benki hiyo ambazo zina manufaa makubwa.
0 comments:
Post a Comment