Yusuf Manji
MASHABIKI
wa Simba wamekuwa wakiwakebehi watani zao, Yanga kuhusu uwanja wao wa
Kaunda, uliopo Jangwani, hasa baada ya kupata eneo kubwa huko Bunju
ambako wameanza makeke wakitengeneza uwanjani wao wa kisasa.
Kumbe
bosi wa Yanga, Yusuf Manji alikuwa akizisikia kebehi hizo na kuamua
kufanya jambo moja ambalo ni kama jibu kwa Wana Msimbazi, baada ya
kugawa eneo lake la ardhi lililopo Kigamboni na kuipa Yanga ili ijenge
uwanja baab’kubwa.
Jana
Jumatano klabu hiyo ilizindua eneo hilo itakalojenga uwanja huo huko
Gezaulole, Kigamboni pembezoni mwa jijini la Dar es Salaam.
Kiwanja
hicho cha Manji chenye ukubwa wa Hekta 712 kimemegwa na kukabidhiwa kwa
Yanga, ambapo uzinduzi wa jiwe la msingi ulifanywa na Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Mama Fatuma Karume.
Waziri
Nchemba alisema amefurahishwa na hatua ya Manji kuonyesha usikivu na
kukubali ushauri aliowahi kumpa kuachana na fikra za kujenga uwanja eneo
la Jangwani na kumtaka atafute maeneo ya nje ya mji kama walivyofanya
Simba waliokimbilia Bunju.
Alisema
anaamini uwanja huo utakuwa machinjio ya wapinzani katika Ligi Kuu na
kwamba, uwanja kujengwa Gezaulole, neno ambalo kwa kizaramo lina maana
ya Njoo Muone.
Kwa
upande wa Mama Karume, ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
ya Yanga, alisema Manji ni kama ameitikia wito wa wanachama waliomlilia
kwenye Mkutano Mkuu wa hivi karibuni waliotaka wajengwe uwanja wao ili
kuepuka kejeli za Simba.
0 comments:
Post a Comment