Muimbaji
huyo ambaye ameachana na uongozi wake wa zamani wa THT, ameonyesha
kuchukizwa na kauli hiyo ya Diva ambapo kila akiulizwa kuhusu kauli hiyo
amekuwa akitoa maneno makali.
“Kuhusu Diva, bora tu niachane naye
maana sioni vitu vya kumuongelea kama anavyofanya yeye,” Ruby aliliambia
gazeti la Mtanzania “Zaidi namuonea huruma tu, namsikitikia na
ninamwombea kwa Mungu amrudishie akili zake. Nahisi ana ugonjwa wa
kusahau, jambo ambalo ni baya sana kulingana na umri wake,”
Pia
muimbaji huyo amesema kwa sasa amefunga ukurasa wa kuzungumzia masuala
ya uongozi wake uliopita huku akidai kwa sasa ana nafasi ya kufanya
vizuri zaidi kimuziki akiwa mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment