Watumiaji wa smartphone au
maarufu Simu-Janja ni watu makini sana linapokuja suala la ukubwa wa simu,
mwenendo wa masoko kwa sasa unaonyesha wanunuaji wengi wa simu wanavutiwa sana simu zenye kioo kipana.
Lakini sio wapenzi wote wa simu wanatamani simu zenye kioo kipana,
watumiaji wengine wanapenda simu zenye ukubwa wa wastani. Fununu zilizotapakaani kuwa
TECNO wanakuletea simu mpya Phantom 6 ambayo pia itakuja na matoleo mengine kama
Phantom 6 Plus naPhantom 6 mini. Fununu hizi zinaweka wazi kwamba watengenezaji hawa wakubwa wa simu za mkononi wanamkakati kabambe wakuwavutia watumiaji wakubwa wa simu kununua matoleo haya mapya yanayotarajiwa kutoka Septemba hii pindi
TECNO Phantom 6 itakapazinduliwa.
HAKUNA SHAKA JUU YA UKUBWA WAKE
Jambo hili linatia moyo huku TECNO ikiwekwa bayana katika uvumi unaosambaa angalau kwa vidokezo na muonekano ambao unasemekana ni rasmi
Tecno Phantom 6 itaboreshwa zaidi na wala haitopunguziwa sifa zake kuu. Nafikiri hili ni jambo
la kufurahisha sana kwasababu mara nyingi tumekuwa tukiona makampuni mengi ya
simu yakiwauzia wateja wao simu zenye uwezo mdogo katika maduka yao makubwa wakitumia jina
la makampuni yanayobamba kwa kuuza simu. Watumiaji wengi wa simu siku hizi wako makini sana na hawadanganyiki kirahisi.
PHANTOM 6 NA MATOLEO MAPYA YA TECNO YATAKUWA NI GUMZO?
Watengenezaji hawa wakubwa wa simu zaTECNO wamekuwa wakipambana kuweka toleo
lao bora kabisa kwenye mauzo kuanzia Phantom A+ mpaka Phantom Z au Z mini,
Phantom 5 na sasa Phantom 6. Swali linalobakini je, phantom 6 itabadilisha
mtazamo wa baadhi ya wananuaji wa simu?
Unadhani wapenzi wa Smartphones wataanza kuiona Phantom 6 kama
moja ya toleo la kipekee kama inavyotarajiwa na wengi? Na inasemekana kuwa Phantom
6 ama 6 + itakamata soko kubwa kipindi hiki endapo toleo zitambulishwa kwa upekee kwa wakati muafaka.
Mbali na fununu zote hizi tunasubiri kuona toleo rasmi
la Phantom 6 kuzinduliwa ifikapo Septemba.
Endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamiiya
Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ
0 comments:
Post a Comment