
Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education
Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika semina ya wazazi na
wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka leo kwenda vyuo vikuu vya nchini
China, iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wanaokwenda nje wakichukua
tiketi pamoja na viza kwa ajili ya safari kwenda katika vyuo vikuu vya
nchini China iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wazazi na wanafunzi
wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Globa Education Link (GEL),
Abdulmaalik Mollel hayupo pichani katika semina iliyofanyika katika
ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.
MKURUGENZI Mtendaji wa Globa Education
Link (GEL), Abdulmaalik Mollel amesema wanafunzi wanaokwenda nje
waliohitimu masomo katika vyuo vya nje wanatakiwa watafutwe na waajiri
na sio wawe wa kutafuta ajira.
Mollel ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa semina na wazazi na wanafunzi 200 wanaotarajia kuondoka leo katika vyuo vikuu vya nchini China, amesema kuwa kutokana na vyuo hivyo kuwa na vifaa vya kujifunzia wanafunzi wakitumia vizuri katika soko la ajira watatafutwa.
Mollel amesema nchi haina tatizo la ajira
hivyo watu wanatakiwa kuwa na uwezo binafsi ambao utamfanya mwajiri
kutafuta mtu wa kumuajiri hivyo wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo
wanatakiwa kutumia maarifa ya kuja kuzalisha nchini.
Amesema wazazi watumie muda wao katika
kuwafuatilia watoto wao wanaosoma nje ili kuweza kuona thamani ya fedha
wanazozitoa na elimu wanayoipata.
Aidha amesema kuwa wale ambao wanahitaji
vyuo vya nje bado nafasi zipo na wanafunzi wote watafuata taratibu zote
ikiwa ni pamoja Tume ya Vyuo Vikuu nchini kujiridhisha na vyuo
wanavyokwenda. Mollel amesema haitakuwa tayari kuona wanafunzi
wanahitimu vyuo vya nje kupitia GEL kuwa hawatambuliki.
Source:- Mjengwa Blog
0 comments:
Post a Comment