STAA wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma na meneja wake, Bond Suleiman
mapenzi yao yamerejea upya baada ya miezi kadhaa nyuma Wastara kumtosa
na kwenda kuolewa na Mbunge wa Jimbo la Donge-Zanzibar, Sadifa Juma.
Kurejea kwa penzi la wawili hao kulibainika baada ya hivi karibuni
waandishi wa habari hii kufika nyumbani kwa Wastara maeneo ya Magereza
Relini jijini
Dar na kumkuta Bond akiwa amejaa tele huku wakioneshana mahaba ya
Dar na kumkuta Bond akiwa amejaa tele huku wakioneshana mahaba ya
njiwa.
Wastara
afunguka Licha ya kwamba mwanzo zilipovuja taarifa kuwa wamerudiana
walikuwa wakitumia nguvu kubwa kukanusha, safari hii walipobambwa
hawakuwa na ujanja zaidi ya kuamua kuanika kila kitu kweupe. “Kweli
tumeamua kurudi kwenye penzi letu na sikutaka kufunguka mapema kwa
sababu siyo kila uhusiano unaufungukia kwani si kila mtu anayependa,
nimepitia matatizo mengi na sababu kubwa ni wanadamu hivyo sikuona haja
ya kutangaza tena huu uhusiano. “Niliamua kurudi kwa
Bond kwa sababu kiukweli ni mwanaume anayependwa na watoto wangu na anajua mwanamke anataka nini,
mengine ni mipango ya Mungu,” alisema Wastara.
AIZUNGUMZIA
NDOA Akizungumzia mipango ya kuoana, Wastara alisema kwa kuwa kila
jambo anayepanga ni Mungu ni vyema akaachiwa yeye. BOND NAYE ANENA Bond
alipotakiwa k u z u n g u m z i a kurejea upya kwa penzi hilo alisema
kwa kifupi: ”Jamani Wazungu wanasema, true love never die… (mapenzi ya
kweli kamwe hayawezi kufa).”
0 comments:
Post a Comment