Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.Waziri
huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi
baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wa nchi hiyo Kim
Jong-un.Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya
muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti
moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa
kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege.Gazeti hilo lilisema wawili
hao waliuawa mapema mwezi huu.
Mapema mwezi huu, naobu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Kusini.

0 comments:
Post a Comment