Posted by Williammalecela.com on Friday, September 23, 2016
Aliyekuwa Waziri
wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga jana aliponda aina ya ndege mpya
zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada kwa ajili ya kufufua Shirika la
Ndege Tanzania (ATCL). Kitwanga alisema ndege hizo si tu hazina mwendo, lakini pia ilikua ni
ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa
kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.
Charles KitwangaSerikali imelipa kwa Bombardier Aerospace fedha za ndege mbili za
Q400 zinazotumia injini ya pangaboi zenye uwezo wa kubeba abiria 70. Kitwanga ambaye ni mbunge wa Misungwi (CCM), alieleza kushangazwa na
kitendo cha serikali kununua ndege hizo ambazo amesema zimetoka katika
kampuni ndogo ya mtu binafsi, na kuhoji ubora wake. Aidha Kitwanga
alisema Tanzania itakua mteja wa kwanza wa ndege hizo. Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa wikipedia, kampuni
hiyo imetengeneza zaidi ya ndege 1,000 za aina hiyo tangu ianzishwe
mwaka 1984, na inatarajia kuwa imetengeneza jumla ya ndege 1,192 ifikapo
mwisho wa mwaka huu. Kitwanga alisema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
ilipokutana na ATCL, na Mamlaka ya Usafiri wa wa Anga (TCAA) mjini
Dodoma. Source: Nipashe
0 comments:
Post a Comment