Bodi
ya wadhamini CUF imefungua maombi ya kufungua kesi katika Mahakama Kuu
dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Jaji Francis Mutungi, Prof Ibrahim
Lipumba na wanachama 12 waliosimamishwa uanachama wa chama hicho.
Katika
maombi hayo bodi hiyo inaomba kibali cha kufungua kesi dhidi ya
Msajili, Lipumba na wenzake, ili mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili
asifanye kazi nje ya mipaka ya mamlaka yake kisheria.
Jana
wajumbe wanne wa bodi hiyo waliibuka na kuunga mkono msimamo wa msajili
wa vyama vya siasa na kupanga kuwakutanisha Profesa Lipumba na Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif ili kumaliza mgogoro.

0 comments:
Post a Comment