Leo
nakuletea orodha ya watu kumi hatari zaidi duniani. Wanatafutwa
kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu waliyowahi kuyafanya dhidi ya
binadamu na mali zao. Baadhi yao tayari wamekamatwa.
10.AYMAN AL-ZAWAHIRI
Mbabe
huyu alikuwa kiongozi wa kundi la Egyptian Islamic Jihad lenye makazi
yake jijini Cairo, Misri. Ndiye kiongozi wa juu wa sasa wa kundi hatari
la kigaidi la Al-Qaeda.
Uhusiano
wake wa karibu na gaidi Osama Bin Laden aliyeuawa mwaka 2012 na majeshi
ya Marekani ndiyo ulipelekea achaguliwe kuwa kiongozi wa juu wa kundi
hili.
Anatajwa
kuhusika na ulipuaji majengo ya Pentagon nchini Marekani na mwaka 2012
alitoa waraka wa kutekwa kwa watalii wote wenye uraia wa nchi za Ulaya
wanaotembelea nchi za Kiarabu.
09.OMID TAHVILI
Anashika
namba tisa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa zaidi duniani kwa makosa
ya uharifu. Ndiye kiongozi wa kundi hatari la uhalifu la Persian Crime
Group lenye makazi yake nchini Canada. Mwaka 2007 alifungwa jela na
alifanikiwa kutoroka huku akiacha maswali mengi. Anahusishwa na wizi wa
pesa na mtandao wa pesa feki nchini Marekani.
08. FELICIAN KABUGA
Mzee
huyu anatajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka
1994 ambapo watu zaidi ya milioni moja waliuawa. Inasemekana amejificha
nchini Kenya na juhudi zote za kumkamata zimeshindikana.
07. JAMES BULGER
Bulger
ni mhalifu sugu nchini Marekani akihusishwa na biashara ya madawa ya
kulevya na mauaji ya raia wasio na hatia. Anatajwa kuhusika kwenye
matukio ya mauaji zaidi ya 19. Anatafutwa na polisi kwa zaidi ya miaka
30 mpaka sasa na anatajwa kuwa na utajiri unaofikia paundi milioni 18.
- ALIMZHAN TOKHATHOUNOV
Mafia
huyu raia wa Urusi anatajwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya,
utekaji nyara na mauaji ya watu mbalimbali. Anatafutwa na nchi yake na
juhudi za kumpata hazijawahi kufanikiwa.
05. JOSEPH KONY
Mpiganaji
wa msituni na kiongozi wa kundi la waasi la Lord Resistance Army. Kony
raia wa Uganda anayetafutwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa, anatajwa
kuhusika kwenye mauaji ya raia wengi wasio na hatia, ubakaji na uporaji.
Anatafutwa tangu mwaka 1986.
- SEMION MOGILEVICH
Anafahamika
kwa jina la ‘Mhalifu hatari zaidi duniani’, anatajwa kuwa kiongozi
mkuu wa kundi la mafia la nchini Urusi linalohusika na mauaji mbalimbali
na biashara ya madawa ya kulevya.
03. DAWOOD IBRAHIM
kiongozi
mkuu wa Indian Crime Network kundi hili la wahalifu maarufu kwa jina la
D-Company linajihusisha na mauaji ya raia, utekaji, ubakaji na biashara
ya madawa ya kulevya kwenye nchi za Pakistan, India na Falme za
Kiarabu. Anatajwa kama mmoja wa washirika wa karibu wa kundi la
Al-Qaeda.
- MATTEO MESSINA DENARO
Anashikiliwa
nchini kwake Italia baada ya kutafutwa kwa miaka zaidi ya ishirini,
japo amekamatwa ili kujibu tuhuma zinazo mkabili bado anahitajika nchi
mbalimbali duniani kwa kuhusishwa na biashara halamu za madawa ya
kulevya na utekaji.
01. JOAQUÍN GUZMÁN
Huyu
ndiye mtu hatari zaidi duniani, maarufu kwa jina la El Chappo, kwasasa
anashikiliwa nchini kwake Mexico. Mara zote akikamatwa huwa anatoroka,
anatajwa kuwa na kikosi hatari kinachojihusisha na biashara haramu ya
madawa ya kulevya, huko nchini Marekani wanamtafuta ili wamnyonge.
Mbali
na uhalifu wake pia ni tajiri anayemiliki kiasi kikubwa cha pesa
kutokana na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya. Anahesabika kama
mhalifu mwenye nguvu zaidi duniani.
Na Leonard Msigwa/GPL.










0 comments:
Post a Comment