BAADA
ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu ujauzito alionao mrembo
anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na
kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika.
Diamond
aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka hayo
kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya Clouds
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine
aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri
kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika.
“Mimi
mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena
imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia
aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho.

Mimi
si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa sijui kama
ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea arudi
katika hali yake ya kawaida,” alisikika Diamond. Ijumaa Wikienda
lilimvutia waya Mobeto ili kuweza kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu
hiyo, simu yake iliita bila majibu.
Ujauzito
wa Mobeto ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi
waliamini mhusika ni Diamond kitendo ambacho kilisababisha maneno
kumfikia mpenzi wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na
kutibua hali ya hewa lakini kwa sasa mambo yako shwari baada ya Zari
kuelewa kwamba Mobeto hana madhara
0 comments:
Post a Comment