Multichoice Tanzania imedhamini
wateja wake 6 walioshiriki kwenye mashindano redioni. Washindi hao wataenda
kuhudhuria tamasha la mziki la MAMA’s, litakalofanyika mjini Johannesburg
Afrika Kusini mnamo tarehe 22, Oktoba,
2016. Tamasha hilo maarufu la mziki linafanyika kila mwaka, na DStv ni
kingamuzi pekee kitakachorusha hewani shindano hilo maarufu la mziki kupitia
chaneli yake ya mziki ya MTV-base 322, saa 4 usiku, mubashara.
Tanzania kwa mashindano ya mwaka huu inawakilishwa
na Navykenzo, Diamond, Alikiba & Sauti Sol, Yamoto band, Vanessa Mdee na
Rayvan . Ambao ni wasanii walioteuliwa kuwania tuzo hizo. Watanzania wanahimizwa
kuwaunga mkono wasanii wetu kwa kuwapigia kura kwenye mitandao ya kijamii kama
Facebook, Twitter na Instagram, na tovuti ya http://mama.mtv.com/voting/. Huduma ya DStv itatuwezesha kutazama tamasha hilo la
mziki huku tukiwashangilia wasanii wetu.
Mkurugenzi mtendaji Maharage Chande,
alisisitizia umuhimu wa kuwaunga mkono washiriki wetu kupitia huduma ya DStv
premium, ili kuweza kubudurika na tamasha hilo la mziki. Hoja hii iliungwa mkono
na wasanii waliohudhuria mkutano huo wa vyombo vya habari kwenye ofisi za
Multichoice.
MKURUGENZI MTENDAJI WA MULTICHOICE
TANZANIA NA WASHINDI WA TUZO ZA AMVCA
2016, WAHIMIZA WATANZANIA KUSHIRIKI KWENYE MASHINDANO YA AMVCA YA 2017.
Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice
Tanzania akiongelea mashindano ya Africa
Magic Viewer’s Choice Award (AMVCA)
kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema “ Africa Magic Viewers Choice
Awards ni tuzo maarufu barani Afrika, zenye lengo la kutambua na kusheherekea
kazi na mchango mkubwa unaotolewa na watengeneza sinema, wacheza sinema na
mafundi mitambo katika tasnia ya filamu na televisheni. Washindi wa tuzo hizi
wanaheshimika Afrika nzima na kuzawadiwa taji la ushindi katika hafla kubwa
inayofanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu, hafla hiyo itafanyika Machi 3-4, 2016.”
Mr. Maharage Chande aliendelea kusema
“Tanzania tuna sababu kubwa ya kushiriki na kuamini kwamba tuna uwezo wa kushinda
tuzo hizo. Kwani mwaka huu tulikuwa na washindi wawili, single Mtambalike
kupitia filamu yake ya “Kitendawili” iliyokuwa filamu bora ya lugha ya
Kiswahili, na Elizabeth Michael kupitia filamu yake ya “Mapenzi” iliyoshinda
filamu bora ya Afrika Mashariki.
Tumejaribu, tumeweza, sasa tujaribu
tena mwaka huu kwa kuwasilisha filamu zetu ambazo tunaona zina uwezo wa
kushinda. Kushiriki ingia kwenye tovuti ya http://www.amvca2017.com, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha
filamu zetu ili zishindanishwe ni tarehe 28, Oktoba 2016.
Mashindano haya hushindanisha wasanii
kwenye maeneo 27, miongoni mwa maeneo hayo ni wacheza filamu, mafundi wa
mitambo, na filamu zenyewe, filamu nzuri
ya Kiswahili, wahariri wa picha, na wahandisi wa sauti za filamu. Katika hafla
hiyo, msanii Single Mtambalike alihimiza watanzania wenzake kutosita kushiriki
kwenye mashindano hayo kwa kutuma kazi zao ili kuitangaza na kuiendeleza vizuri
sanaa ya Tanzania.
Multichoice Tanzania kupitia huduma
zake maarufu za DStv, imekuwa katika mstari wa mbele kuiburudisha jamii kwa vipindi tofauti. DStv ilirusha
hewani tamasha la Africa Magic Viewers Choice Awards ya Machi 5, 2016
iliyoandaliwa na Multichoice Africa.
0 comments:
Post a Comment