Rais John Magufuli akiwa na Mfalme wa Morocco, Mohamed V1 baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini
Dar es Salaam jana.
Picha na Anthony Siame
Dar es Salaam.
Mfalme Mohammed VI wa Morocco amewasili nchini akiwa na msafara wa
ndege tano zilizobeba vifaa vyake, ikiwamo kitanda na mazulia ya
kifalme.
Mfalme Mohammed aliwasili jana saa 11:15 jioni akiwa na ujumbe wake wa watu zaidi ya 150, wakitokea nchini Rwanda.
Kabla ya kuwasili kwa ndege yake, zilitangulia ndege mbili ndogo za Morocco zilizokuwa na ujumbe ulioambatana naye.
Awali,
Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga alinukuliwa akisema msafara
wa Mfalme huyo ulitanguliwa na ndege mbili zilizobeba vitu mbalimbali
kwa ajili ya matumizi yake kwa kipindi chote atakachokuwapo nchini.
“Nadhani
mnajua mapokezi ya kifalme yalivyo, wenzetu wanapenda kuandaa wenyewe
kila kitu atakachotumia mfalme wao. Ndege mbili zimewasili zikiwa
zimebeba vifaa mbalimbali vikiwamo kitanda na mazulia ya kifalme,”
alisema Dk Mahiga kabla ya ujio wa Mfalme Mohammed VI.
Mfalme
Mohamed VI alipokewa uwanja wa ndege na vikundi mbalimbali vya burudani
na raia wa Morocco wanaoishi nchini. Ulinzi uliimarishwa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa maofisa usalama wa
pande zote mbili kwa kuzunguka pande zote za uwanja huo.
Source:- Mwananchi Blog
0 comments:
Post a Comment