Njemba huyo akisihi kuachiwa baada ya sakata hilo.
NI aibu iliyoje! Mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, amekutwa ndani ya danguro moja lililopo Sinza ya Mapambano jijini Dar ikiwa ni mazingira ya kutatanisha.
Ishu
hiyo ilijiri usiku wa manane wa Ijumaa kuelekea Jumamosi ya wiki
iliyopita. Awali, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
ilipokea taarifa kutoka kwa vyanzo vyake kuwa ndani ya danguro hilo,
ameingia mwanaume huyo aliyeonekana kuwa na heshima zake na kwa vile
inaeleweka vitu vinavyoendelea, vyanzo vilikuwa na wasiwasi naye!Bila
kupoteza muda, kikosi kazi
cha
OFM kilifuatilia eneo hilo na kufanikiwa kuingia ndani ya danguro hilo
ambako walimkuta jamaa huyo akiwa anazungumza na wasichana watatu ingawa
haikueleweka mara moja walikuwa wakizungumzia nini.
Baada
ya kuwaona makamanda wa OFM, waliacha mazungumzo yao na kuwatumbulia,
lakini walipoanza kupigwa picha, ukaibuka mzozo mpya baina ya watu hao
wakisaidiwa na walinzi wanaolinda danguro hilo, dhidi ya waandishi.
0 comments:
Post a Comment