Dar es Salaam.
Wakati Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi Dar es Salaam (Dart) ukiwa
umefikisha siku 158 tangu ulipozinduliwa Mei 10, kampuni inayouendesha
imelazimika kupunguza wafanyakazi kutokana na gharama za uendeshaji kuwa
kubwa.
Nauli
za mabasi hayo yaliyolenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam,
zilitangazwa Mei 9, ikiwa ni siku moja kabla ya uzinduzi wa safari zake.
Nauli
hizo zilizotangazwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri
Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Johansen Kahatano ni Sh800 kutoka Mbezi
Mwisho hadi Kivukoni na wanafunzi ni Sh200.
Nauli
kutoka Mbezi Mwisho-Kimara hadi Kariakoo Sh800 na Kutoka Morocco -
Kimara hadi Mbezi Mwisho ni Sh800 na kutoka Morocco - Kivukoni Sh650,
sawa na Kariakoo hadi Morocco.
Lakini
nauli hizo zinazonekana kutokidhi gharama za uendeshaji. Katika
kutathmini siku 158 tangu kuanza kwa huduma hiyo, Mwananchi ilizungumza
na David Mgwassa, mkurugenzi mtendaji wa Udart inayoendesha mradi huo
ambaye alisema gharama za uendeshaji ni kubwa kuliko mapato.
“Kwa
siku tunapakia abiria 120,000, lakini gharama za uendeshaji ni kubwa
kuliko mapato kwa sababu nauli tuliyopewa ni chini ya ile tuliyoomba na
iliyowekwa kwenye mkataba,” alisema Mgwasa.
Source:- Mwananchi Blog
Source:- Mwananchi Blog
0 comments:
Post a Comment