Gigy Money.
Hali
ngumu na raha ya ubuyu usimung’unye mwenyewe! Ishu inayotrendi kwa sasa
kwenye ulimwengu wa ubuyu wa mjini ni aibu ya baadhi ya mastaa wa kike
Bongo kudaiwa kuwanasa wanaume mtandaoni kwa njia ya picha zinazoonesha
sehemu kubwa ya miili yao.Kufuatia
ishu hiyo, kumeibuka malalamiko kwamba, picha hizo haziishii tu
mitandaoni bali zinawafikia hata watoto wao na kumomonyoa maadili ya
Kitanzania kwani baadhi ya watu, wakishavutiwa nazo, huzichukua na
kutumiana kwenye simu hivyo kusambaa kwa watu wengi zaidi.Chanzo
makini ambacho ni mfuatiliaji wa karibu wa ishu za mastaa kimeeleza
kwamba, baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakisingizia kuwa wanatangaza nguo
hasa za ndani ndiyo maana huvaa kihasara.

UGUMU WA MAISHA?
Lakini
nyuma ya pazia, inadaiwa kuwa kutokana na ugumu wa maisha kwa sasa,
ndiyo mbinu mpya ya kujipiga promo kwa ajili ya kujiuza kwa wanaume
ambao huwatafuta baada ya kuona picha hizo. “Ninyi hamjui tu! Kama
hamuamini, chunguzeni, wasichana kibao wa mjini pamoja na baadhi ya
mastaa wamebuni njia rahisi ya kujiuza mitandaoni. “Wanachokifanya ni
kwenda studio na kupiga picha kali zinazoonesha maungo yao kisha
wanatupia mitandaoni.
WAWILI WATANGAZA MAFANIKIO
“Kuna
wawili (mastaa) ambao ni marafiki zangu, wanasema wamefanikiwa kupata
dau kubwa kwa siku kutoka kwa wanaume kwa sababu tu ya kujipigia promo
wenyewe,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.
WALIOTAJWA HAWA HAPA
Baadhi
ya mastaa wanaotajwa kujipigia promo kwa wanaume ni pamoja na Isabela
Mpanda ‘Bella’, Hamisa Mobeto, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Auggen
‘Amber Lulu’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Husna Maulid, Faiza Ally Lulu
Semagongo ‘Aunt Lulu’, Mwanaisha Said ‘Dyna’ na Tunda Sebastian.
UBUYU YABAINI KITU
Kufuatia
sakata hilo, Kona ya Ubuyu Ulionyooka ilizungumza na baadhi ya mastaa
waliotajwa ambapo wapo waliokiri kuwa, biashara hiyo inalipa zaidi kwani
haina gharama lakini pia walidai kuwa kila mtu ana maisha yake na
anajua anapopatia mkate wake wa siku bila kujali kujiondolea utu.
MSIKIE GIGY:
“Kama
inalipa, haimhusu mtu, ninachojua ni kweli wapo wanawake wengi
wanaojiuza, cha muhimu ni kujua dau lako na siyo kufuatilia maisha ya
wengine, mimi naishi maisha yangu.
” HUYU HAPA BELLA
Kwa
upande wake Bella alifunguka kuwa, yeye si wale waliopo kwenye kundi
hilo ila anapenda tu kupiga picha hizo kwa sababu ya mwili alionao na
pia ikumbukwe kuwa aliwahi kuwa miss na kazi yake ya muziki na uigizaji
vinamruhusu.
TUNDA ANAFUNGUKA:
“Mimi
napenda kufanya nitakacho, siangalii watu wanataka nini ILIMRADI ni
ukurasa wangu, siwezi kuzuiwa kufanya lolote. Kuhusu wanaume, hata
wakija wengi huwa nawapotezea tu na wala hawajakosea kwa sababu wapo
wanaodhani tunapiga picha kwa ajili hiyo na kutuma komenti kibao.” Hao
ni baadhi ya mastaa waliopatikana na kupewa nafasi ya kujitetea lakini
katika uchunguzi wa Wikienda, ilibainika kuwa wengi wanaoweka picha
hizo, lengo lao huwa ni kutangaza nguo kama walivyowahi kujitetea Hamisa
Mobeto, Lulu na wengineo.
NENO LA MHARIRI
Siyo
hukumu ya Wikienda wala msomaji wake kuwa mastaa wanaotajwa ni kweli
kwamba wanajiuza kwa njia hiyo lakini kama kweli wanafanya hivyo,
wanapaswa kujiheshimu kabla ya kuumbuliwa kwani kila mmoja anajua kwamba
tukimvalia njuga tutamuumbua. Kama ni suala la matangazo ya nguo, basi
wafanye matangazo kwa wakati kisha kujiweka kiheshima na siyo kila nukta
kutupia picha za nusu utupu. Pia kama ishu ni kukosa wachumba,
wakumbuke kuwa ndani ya mitandao hiyohiyo kuna uwezekano wa kuwepo kwa
wachumba na wakwe hivyo ni rahisi kupoteza sifa za mke bora.


0 comments:
Post a Comment