Posted by Williammalecela.com on Wednesday, October 12, 2016
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa
wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican kuondoa rasmi uungaji
mkono wao kwa mgombea wa chama hicho Donald Trump.
Akiongea katika
mkutano wa kampeni wa kumuunga mkono mgombea wa chama cha Democratic
Hillary Clinton, Bw Obama amesema haina maana kukemea matamshi ya
kudhalilisha ya Bw Trump kuwahusu wanawake bila kujitenga na mgombea
huyo. Akihutubu Greensboro, North Carolina, Jumanne jioni, Rais
Obama alishangaa ni vipi wanasiasa wa Republican bado wanataka Bw Trump
awe rais. "Hali kwamba sasa kuna watu wanaosema: 'Sikubaliani
kamwe na hili, napinga hilo kabisa ... lakini bado tunamuidhinisha.'
Bado wanafikiri anafaa kuwa rais, hilo kwangu halileti maana," alisema. Bw Obama alisema matamshi ya Bw Trump kuhusu wanawake hata yanaweza kumfanya akose hata kazi ya dukani. "Sasa
unapata hali ambapo huyu bwana anasema mambo ambayo hakuna anayeweza
kuyavumilia hata kama mtu huyo angekuwa akiomba kazi (maduka ya)
7-Eleven," alisema. Bw Obama alikatizwa mara kadha akitoa hotuba
na wapinzani wa Bi Clinton lakini alionekana kutoathirika. Badala yake
aliwajibu: "Hii ni demokrasia. Hili ni jambo zuri sana." Watu hao waliokuwa wakimzomea walitolewa nje na maafisa wa usalama.
Maafisa wengi wakuu wa chama cha Republican, akiwemo spika wa
bunge la wawakilishi Paul Ryan ambaye ndiye afisa wa ngazi ya juu zaidi
wa chama hicho aliyechaguliwa, wameshutumu matamshi hayo ya Bw Trump
ambaye anaonekana akijigamba kuhusu kudhalilishwa kwa wanawake kwenye
video. Image copyrightAFPImage caption
Watu kadha walitatiza hotuba ya Bw Obama
Bw Trump hata hivyo amewashambulia vikali wanasiasa
hao na kusema ni wasaliti, na kwamba inakuwa vigumu kupambana nao kuliko
hata wanasiasa wa chama cha Democratic.
Amesema kwa sasa minyororo iliyokuwa imemfunga imeondolewa na ataipigania Marekani kwa njia anayoitaka.
Image copyrightAPImage caption
Trump amesema wanasiasa wa Republican wanamshambulia kutoka "kila upande"
Mhariri wa BBC wa masuala ya Amerika Kaskazini
anasema kimsingi kwa sasa Bw Trump ni kama anaendesha kampeni yake kama
mgombea huru. Amedokeza kwamba uhasama uliojitokeza kwa sasa utaendelea hata baada ya uchaguzi. Kwenye
kanda ya video ya mwaka 2005 iliyotolewa Ijumaa, Bw Trump anaonekana
akieleza jinsi alivyojaribu kuomba kushiriki ngono na mwanamke
aliyeolewa pamoja na pia kutoa matamshi mengine ya kuudhi kuhusu
wanawake. Karibu nusu ya maseneta, magavana na wabunge wote 331 wa
Republican wameshutumu matamshi hayo ya video na karibu asilimia 10
wametoa wito kwa Bw Trump kujiondoa, kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters.
Bw Trump hata hivyo amewashambulia vikali wanasiasa hao na kusema ni
wasaliti, na kwamba inakuwa vigumu kupambana nao kuliko hata wanasiasa
wa chama cha Democratic.
Amesema kwa sasa minyororo iliyokuwa imemfunga imeondolewa na ataipigania Marekani kwa njia anayoitaka. Mhariri wa BBC wa masuala ya Amerika Kaskazini anasema kimsingi kwa
sasa Bw Trump ni kama anaendesha kampeni yake kama mgombea huru. Amedokeza kwamba uhasama uliojitokeza kwa sasa utaendelea hata baada ya uchaguzi. Kwenye
kanda ya video ya mwaka 2005 iliyotolewa Ijumaa, Bw Trump anaonekana
akieleza jinsi alivyojaribu kuomba kushiriki ngono na mwanamke
aliyeolewa pamoja na pia kutoa matamshi mengine ya kuudhi kuhusu
wanawake. Karibu nusu ya maseneta, magavana na wabunge wote 331 wa
Republican wameshutumu matamshi hayo ya video na karibu asilimia 10
wametoa wito kwa Bw Trump kujiondoa, kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters.
0 comments:
Post a Comment