Posted by Williammalecela.com on Friday, October 21, 2016
 |
UVCCM Wakutana na Mkurugenzi Bodi ya Mikopo Tanzania
Kutokana na Vuguvugu la Swala la Mikopo katka vyuo vya Elimu ya juu Tanzania kuto kuekeweka
Mapema ya Leo Viongozi wa Umoja wa Vijana Chama (UVCCM) Wakiongozwa na
Mtemi Sylvester Yaredi Kaimu mkuu idara Uhamasishaji sera utafiti na
mawasiliano Uvccm Taifa Akifuatana na Tumain Mwakasege kaimu mkuu Idara
Uchumi Fedha na Uwezeshaji Uvccm.
wamekutana na Kufanya Mazungumzo ya kina na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania Ndg:Abdul Razaq Badru.
Katika Mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania Ndg:Abdul
Razaq Badru alitoa Ufafanuzi juu ya taratibu,Sifa na Vipaumbele mbali
mbali vya Serikali juu ya Mwanafunzi atakae pata Mkopo.
Aidha
katika Mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania Ndg:Abdul
Razaq Badru alitolea Ufafanuzi juu ya idadi ya Majina ya Wanafunzi 3000
ambao alisema ni batch ya kwanza na ni kwa vyuo vya DAR tu . nakuomba
jamii kuepuka upotoshwaji unaoendelea katika baadhi ya Mitandao na
kusema Idadi halisi kwa Wanafunzi Wanaotakiwa kupokea Mkopo huo ni
Wanafunzi 21500."tunashangaa kusemwa tumetoa mikopo kwa wanafunzi 3000
tu ilihali hao ni batch ya kwanza kwa vyuo vya Dsm tu vivyokwisha
kufunguliwa ikiwemo UDSM"
Pia kwa Upande wa UVCCM ndg:Mtemi
Sylvester Yaredi Kaimu Katibu Idara ya Hamasa,Sera na Utafiti na
mawasiliano aliiomba Bodi ya Mikopo kutazama na kuongeza juu ya pesa za
_MEALS AND ACOMODATION___kwa Wanafunzi kwasababu ya hali ya Maisha
Vyuoni.
"Alisema Yaredi kama Umoja wa Vijana tunaiomba bodi ya
Mikopo kutazama kwa mapana zaid juu ya kiasi Cha awali kilicho tolewa
na Bodi kwani ni kidogo sana ukitazama na Maisha ya Mwanafunzi hii
itasababisha Wanafunzi kushindwa kutimiza Mambo mbali mbali pindi wawapo
Vyuoni".
Katika Mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo
Tanzania Ndg:Abdul Razaq Badru ameihakikishia UVCCM kuwa itakamilisha
Taratibu zote na Kutangaza Majina ya Idadi Wanafunzi wote watakaopata
Mkopo huo ifikapo Siku ya
Jumamosi na kueleza ya kuwa bodi ya mikopo
imezingatiaVipaumbele vya Kitaifa katika Utoaji wa Mikopa na zaidi ya
waombaji 6000 wenye mahitaji maalum watapata mikopo kwa asilimia 100% Ambao ni Yatima na walemavu waliowasilisha vielelezo.
Kesho UVCCM Itafanya kikao chake na Waziri wa Elimu na Siku ya Juma
tatu UVCCM inatarajia kukutana na Waziri wa Fedha na Uchumi.
..... |


0 comments:
Post a Comment