Sahihi ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika
kama inavyoonekana katika Barua ya maazimio ya Bodi ya wakurugenzii ya
kampuni ya TESTA LIMITED ili kukopa katika benki ya Standard Chaterd
kiasi cha mkopo wa milioni 300. mkopo ambao mnyika amekana kuhusika nao.
John Mnyika.
Na. Mwandishi wetu,
wakati Mbunge wa Kibamba na naibu katibu mkuu wa Chadema John John
Mnyika akikana kuutambua mkopo wa milioni 300 uliokopwa na kampuni
inayohusishwa kumilikiwa naye ya TESTA LIMITED huku yeye akiwa kama
mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi mwenye mamlaka yote ya kiutendaji
katika kampuni hiyo.
hali sasa imebadilika baada ya siri zaidi kuhusiana na ushiriki wa
mbunge huyo machachari kukopa kiasi hicho cha pesa kuanza kuwekwa
hadharani.
vielelezo vya kikampuni, kibenki na kimalipo ya mkopo huo na mingine
kadhaa inayoihusu kampuni hiyo, vinaonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa
mbunge huyo kijana.
katika mkopo unaohusisha udhamini wa nyumba ya Erasto Tumbo ambaye
wakati anaidhamini kampuni hiyo ya mnyika, alikuwa Afisa wa Uenezi makao
makuu ya chadema huku Mnyika yeye akiwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
yaani bosi wake, tumbo yeye nyumba yake ilithaminishwa kwa shilingi
milioni 160 na shilingi 140 zilizosalia zilisaminishwa na nyumba ya Mzee
Charles Tumaini Chanika ambaye pia ni Meja Mstaafu wa Jeshi la wananchi
wa Tanzania.
Taatifa zinasema kuwa Mnyika na Wenzake waliomba mkopo huo kwa ajili ya
kufanyia biashara zao na kwamba yeye mnyika akiwa kama Mwenyekiti wa
Bodi Kampuni alitoa Dhamana ya Hadhi yake (Personal Guarantee) ya
shilingi milioni 300, sambamba na mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bwana
Lazaro Obadia Mtani aliyetoa pia dhamana kama hiyo.
vielelezo vinasema hati hizo zilisainiwa na mnyika, Mtani na madirisha
mbele ya mwanasheria wa kampuni hiyo Thomas Brash tarehe 11 mwezi wa
Tano 2012.
baada ya kusainiwa kwa hati hizo ziliwasilishwa benki na kupatiwa mkopo
huo tarehe 14.08.2012 na kuanza kurejesha rejesho la jumla ya shilingi
milioni tisa na laki moja na elfu ishirini kuanzia tarehe 21.08.2012.
ambapo mkopo ulipaswa kuwa wa miezi 48 mpaka mwezi Julai mwaka
huu.ambapo katika kipindi chote cha awali ambacho marejesho hayakuwa
yakisumbua Mnyika aliendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa
kampuni hiyo ya Testa.
vielelezo zaidi vinaonyesha kwamba mpaka kufika 31.01.2014, siku ambayo
TESTA ilipeleka rejesho mara ya mwisho na kushoindwa kuweza kulipa tena
huku ikibakisha deni la shilingi milioni 222 na ushee, Mnyika alikuwa
bado mwenyekiti wa Bodi.
taarifa za uhakika ambazo JAMVI LA HABARI linazo, zinasema miezi kadhaa
mbele baada ya kampuni hiyo kushindwa kuendelea kulipa ndipo baadhi ya
watu wanaomzunguka Mnyika walipomshauri Mbunge huyo ajitoe kwenye
umiliki wa kampuni hiyo na kusingizia kuwa siasa zinambana huku ukweli
akiujua kuwa ni kukimbia mrundikano wa madeni .
jambo linaloonekana kushangaza wengi ni kitendo cha mnyika kujitoa kimya
kimya katika umiliki wa kampuni hiyo hasa baada ya kushindwa kulipa
deni bila hata kuwajulisha Tumbo na Meja Chanika ambao walitoa nyumba
zao kumdhamini.
akizungumza na JAMVI LA HABARI mtaalam wa masuala ya fedha Bwana Crispin
Makejo amesema alichokifanya mnyika ni mchezo wa kuigiza na kwamba hana
namna zaidi ya kulipa deni hilo.
'' ukikopa pesa benki, na wewe ukiwa mwenyekiti wa Bodi, na ukasaini
Board Resolition, benki itakuhesabu kama wewe ndiye mkopaji na una
wajibu wa kulipa deni hilo''. anasema Makejo
zaidi makejo anaongeza ''kitendo cha Mnyika kuweka Personal Guarantee,
anajikanganya zaidi na kwamba Personal Guarantee inamuhitaji yeye
kurejesha deni hilo katika hali yoyote ya kipato chake hata kama
amefilisika''.
siku za hivi karibuni Mnyika alinukuliwa na Gazeti mola la Kiswahili
(Sio JAMVI LA HABARI) Kuwa hausiki na kampuni hiyo na kwamba alishajitoa
kwenye kampuni hiyo bila kusema amejitoa lini, na anataka nani amlipie
deni alilokopa yeye mwenyewe.
Taarifa zilizothibitishwa na JAMVI LA HABARI zinasema kuwa Mnyika na
TESTA LIMITED kwa sasa wamefilisika na hawana uwezo tena wa kulipa
madeni hayo na hata meneja msimamini (Mkurugenzi mkuu) wa Kampuni hiyo
bwana Obadia ameshakata tamaa ya biashara ya kampuni hiyo.
''Kinachoniumiza zaidi ni Mnyika kumtumia ndugu nyangu vibaya, kwanini
hakuchukua mkopo kwa nyumba ya Mama yake ya mtoni Kichangani pale.
kwanini anataka kumtia umasikini ndugu yangu?, hatuwezi kukubali hata
kidogo''. anasema ndugu wa mmoja wa wadhamini.
wakati madeni ya Standard Chatered yakifikia sura hii, taarifa zinasema
TESTA LIMITED ikiwa chini ya Mnyika inadaiwa zaidi ya Shilingi bilioni 1
na Benki nyingine Kadhaa.
Mpaka sasa Nyumba inayomilikiwa na Erasto Tumbo, Imeshapigwa Mnada mara
mbili na kwamba jumaapili ya tarehe 02.10.2016 ilikuwa ipigwe mnada kwa
mara ya tatu lakini madalali wanaohusika na suala hilo hawakufika kupiga
mnada japo walitangaza.
JAMVI LA HABARI litaendelea kuwajuza juu ya kadhia hii na nyingine
nyingi zinazowahusu watu wenye vipato vya kawaida na vya chini
wanapoonyesha kutaka kudhulumiwa ama kupotezewa haki zao.



0 comments:
Post a Comment