Imefichuka
kuwa, baadhi ya wanaume kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC)
waliopiga makazi yao Bongo, wamewamaliza mastaa nchini kutokana na penzi
la pesa wanalolimwaga kwao, Uwazi limechimba.
Kwa
mujibu wa chanzo cha karibu na mastaa waliokwishagawa penzi kwa Wakongo
hao, kinachoonekana sasa ni mashindano ya mastaa wa Bongo kila mmoja
kwa nafasi yake kuhakikisha anafaidi pesa za mapedeshee hao licha ya
kwamba, mapenzi yao hayadumu. “Jamani nyie watu wa Global, sidhani kama
mmewahi kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kuhusu hawa wanaume wa
kutoka Kongo. Baadhi yao wamekuwa wakigawa pesa ili kuwapata mastaa wa
Bongo.
“Ndiyo maama ukifuatilia utagundua kuwa, kila kukicha, Mkongo
f’lani kamchukua staa f’lani. Mbaya zaidi, mastaa wanazungukana wenyewe
kwa wenyewe. Leo utasikia Mkongo yupo na huyu, kesho yupo na yule na
wenyewe mastaa wanajua, lakini hawakatai maana wao wanataka pesa tu,”
alisema mtoa habari huyo ambaye naye ni staa lakini asiyetaka
‘kujinajisi’ na jasho la Wakongo hao. Mnyetishaji huyo aliendelea kuweka
wazi kwamba, maisha ya Wakongo hao hapa Bongo ni ya taiming:
“Kuna wakati wanachacha sana. Lakini wakipata ndiyo kufuru yao inakuwa
kwa wenzangu na mimi. Mimi aka! N’takula pesa za mwanaume mwenye mapenzi
na mimi lakini siyo wanaofuata majina makubwa kama fasheni. Nyie
fuatilieni mtagundua mastaa walionasa kwa Wakongo wote wana majina
makubwa, sasa hapo amebaki nani “Halafu hawa jamaa, pesa nyingi
wanazipata kutoka kwenye nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Dubai. Sijui kule
wanafanya dili gani? Ila akitokea amekwenda kule akiwa mchovu, akirudi
hatulali mjini. Kwa kweli pesa ni za kumwaga kwani katika hali halisi,
wanaume hao wanawazidi wa Kitanzania kwa kuhonga. “Wapo mastaa
wanahongwa shilingi milioni ishirini mpaka hamsini. Ndiyo maana unawaona
mastaa wenzangu wengine hawachezi filamu muda mrefu, lakini wanaishi
sawa, wanakula, wanavaa, wanakwenda saluni, wana magari, wanaweka mafuta
na wanafanya bethidei tena za kufuru.”
KUMBUKUMBU YA UWAZI
Kumbukumbu
ya gazeti hili, mpaka sasa, mastaa wa Bongo ambao wameshaandikwa kwenye
magazeti pendwa kuwa wanatoka au wamewahi kutoka na wanaume Wakongo ni
kama ifuatavyo: Wema Sepetu na Husna Idi, wao wameshaandikwa kutoka na
Mkongo aitwaye Mwami Rajab ambapo siku za karibuni, mkewe wa Mwami, Nora
Chilu alijitokeza na kuwapiga mkwara mastaa hao kuachana na mumewe
Jacqueline Wolper, yeye amewahi kuandikwa kutoka na Mwami, lakini
baadaye wakamwagana na kunasa kwa Mkongo mwingine, Putin ila kwa sasa
wememwagana. Hivi karibuni, mwigizaji mwingine Bongo, Shamsa Ford
ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, aliandikwa akidai kuwa, Mkongo wa Wolper
na Wema (hakumtaja jina) amemtongoza
lakini akamchomolea mbali.
Pia,
mwanamitindo mwenye mvuto Bongo, Hamisa Mobeto amewahi kuandikwa kunasa
mtungo wa Mkongo, Mwami. Mobeto alibainika baada ya meseji zake za simu
kunaswa akiomba pesa za kulipia mapazia. Staa mwingine aliyewahi
kuandikwa kutoka na Mkongo huyo ni Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald
‘Masogange’. Pia, aliyewahi kushiriki Bongo Star Search, Baby Joseph
Madaha, hivi karibuni aliandikwa kumzoa bwana wa Wema ambaye ni Mkongo
aliyejulikana kwa jina la John na walilala wote hotelini nchi jirani.
Kuhusu
msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ yeye aliwahi kuandikwa na Mkongo,
Mwami. Mkongo huyo alisema anamtaka msanii huyo kwa gharama yoyote ile.
Lakini siku chache, Lulu alijibu kuwa, kama Mkongo huyo angekuwa na
mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti.



0 comments:
Post a Comment