SIMIYU: Mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imewahukumu kwenda jela miaka kumi watuhumiwa wawili ambao ni miongoni mwa watuhumiwa kumi waliokuwa wakituhumiwa na kesi ya kutungua helikopta ya kampuni ya Mwiba Holings katika pori la Akiba la Maswa Maswa lililoko Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti mwezi January mwaka huu.
Katika tukio hilo aliyekuwa rubani wa helkopita hiyo Roger Gower raia wa Uingereza aliuawa sambamba na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.
Waliokumbwa na hukumu hiyo ni Doto Huja Kubeja na Mwigulu Kanga wote wakazi wa wilaya ya Meatu ambapo katika kesi hiyo walikuwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kumiliki silaha na kumiliki risasai kinyume cha sheria.
0 comments:
Post a Comment