Mwanamuziki
nguli wa muziki wa Dansi nchini, Ally Choki ambae bado anafanya vizuri
kwenye ramani ya muziki wa dansi kutokana na umahiri wake katika nyimbo
zake pamoja akiwa stejini.
Jumamosi hii mwanamuziki wa dansi nchini
tanzania Ali Choki ametimiza miaka 30 ya muziki wake na amewashukuru wasanii ambao
alishirikiana nao katika kipindi chote hicho cha muziki wake.
Akiongea ndani ya eNewz Ali Choki amesema
anashukuru
kwa ‘kampani’ aliyoipata kutoka kwa wanamuziki wenzake kama Zahir Zoro,
Komando Hamza Kalala na wengine lakini pia aliamua kupiga nyimbo za
Extra Bongo ili kuonesha maana ya halisi ya miaka 30 ya Choki.
Hata
hivyo Choki amesema huenda aka pumzika baada ya miaka 20 ijayo mbele
japo hawezi kusema rasmi kwamba ataacha muziki kwa kuwa siyo rahisi
kustaafu muziki kwani muziki ni kipaji chake labda akifikisha miaka 50
ya muziki.

0 comments:
Post a Comment