Noah ikiwa imeharibika-Picha zote na Frank Mshana- Malunde1 blog
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Jumanne Muliro akiwa katika eneo la tukio
Miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio
Noah ikiwa eneo la tukio
Lori likiwa limeharibika
Lori likiwa limeharibika
Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya Noah kugongana na lori
*****
Watu 18 wamefariki dunia na watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah iliyokuwa inatoka Nzega mkoani Tabora kuelekea Tinde mkoani Shinyanga na lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama kuelekea Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea leo Jumapili,November 06,2016 majira ya mbili kasorobo usiku katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga (Barabara ya Nzega- Shinyanga).
"Noah ilikuwa inataka kulipita lori jingine ndipo ikagongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Kahama... watu waliopoteza maisha papo hapo ni 15,watatu wamefariki wakati wakipatiwa matibabu,ajali inatisha,dereva wa Noah kajisalimisha kituo cha polisi Tinde",kimesema chanzo cha habari cha Malunde1 blog.
Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.










0 comments:
Post a Comment