Zikiwa zimesalia takriban siku 53 kufika Novemba 8, mwaka huu, siku
ya Uchaguzi wa Urais wa Marekani, picha za mmoja wa wagombea wake kutoka
Chama Cha Republican, Donald Trump na mwanamitindo wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata zinazowaonesha ‘live’ kwenye redcarpet
zimeibua mambo, Ijumaa linafunguka.
DONALD NA FLAVIANA
Donald
Trump ni mgombea urais tajiri ambaye ni mfanyabiashara aliyefanikiwa
duniani na mwenye kauli tata dhidi ya wageni na matajiri wenzake nchini
Marekani huku Flaviana Matata akiwa ni binti wa Kitanzania aliyetwaa
Taji la Miss Universe Tanzania 2007. Akiwa mmoja wa mamodo wa kimataifa
wenye mafanikio Bongo, Flaviana ambaye ni Mkurugenzi wa Flaviana Matata
Foundation (FMF) kwa sasa anaishi na kufanyia kazi zake za kutangaza
mavazi huko New York nchini Marekani, akiwa amepitia lebo nyingi kubwa
za mavazi za nchini humo.
ATANGAZA NIA, PICHA ZAIBUA
MAMBO Mara baada ya Donald Trump kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo,
hata kabla ya kupitishwa na chama chake dhidi ya mgombea wa Democratic, H
i l l a r y C l i n t o n n d i p o picha hizo zikaibuliwa z i k i w a
na mjadala kabambe kwenye mitandao ya kijamii.
“Halohaloo...
Ndiyo hivyo Flvav (Flaviana Matata) yupo na Donald Trump, Wabongo
hoyeee... “Naona Flaviana yuko na shemela (shemeji) yetu mwenye CV na
utajiri mkubwa duniani tena mgombea urais wa Marekani! “Ninavyojua mimi
Flaviana ni mke wa mtu na aliolewa hivi karibuni ‘so’ hilo tukio na
Trump lilikuwa kabla hajaolewa. “Nina uhakika huyo jamaa akishinda,
Flaviana atakuwa ameulaa maana ni kiasi cha kumtumia tu picha zake na
kumkumbusha walipokutana,” zilisomeka baadhi ya ‘komenti’ za wachangiaji
wa picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.
IJUMAA LATAFUTA UKWELI WA PICHA
K
u f u a t i a m j a d a l a huo, Ijumaa lilizama na kuchimba ili
kutafuta ukweli wa picha hizo a m b a p o l i l i b a i n i kuwa
zilipigwa siku za nyuma huko New York, Marekani katika hafla ya
kumpongeza mshindi aliyekuwa Miss Universe, Fadil Berisha.
NDOA YA FLAVIANA
Flaviana
ambaye ana mafanikio makubwa kupitia ulimbwende kiasi cha kuwa ‘role
model’ wa mabinti wengi Bongo, alifunga ndoa na Deogratius Massawe
Agosti 15, 2015 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na kufuatiwa na
sherehe iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar.

0 comments:
Post a Comment