KAMPUNI ya Maltichoise nchini Tanzania kupitia King’amuzi cha DSTV imefanya mapinduzi ya bei mpya ya vifurushi vyake mbalimbali pamoja na DSTV Bomba kilichopunguzwa kwa asilimia 15 kutoka shilingi 23500 hadi shilingi 19950/=.
Kampuni hiyo yenye kauli mbiu ya zamu yetu imefanya punguzo kubwa la bei na kuongeza idadi ya chanel.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Baracka Shelkindo Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Multchoice, katika uzinduzi wa bei hizo mpya uliofanyika jijini Dar es Salaa, amesema kuwa dhamira yao ni pamoja na kupunguza bei ya vifurushi na kuongeza channel ili kuwanufaisha wateja wao
| ALPHA MRIA MENEJA MASOKO DSTV |
0 comments:
Post a Comment