Muongozaji
wa video na mshindi wa Tuzo za Watu 2015, Hanscana ambae pia ametisha
sana kwenye utengenezaji wa video mpya ‘Muziki’ ya Darasa, pia ndiye
director anayekuja kwa kasi kutokana na ubora wa kazi zake.
Muongozaji
huyo na mtayarishaji wa video nchini Hanscana, amesema sababu inayo
pelekea video nyingi za bongo kurudiwa na kufanana ni kutokana na
maamuzi na mapendekezo ya msanii mwenyewe anacho pendelea.
Hanscana
Akipiga story ndani ya eNewz amesema “Ukiona
kuna kitu kimerudiwa katika video ujue kuna makubaliano kati ya
muongozaji na msanii kwa kuwa mara nyingi msanii anapo andika wimbo wake
anakuwa na wazo la aina ya video ambayo anaitaka hivyo wasanii ni kama
wateja wetu na tunafanya anachokitaka mteja wetu”.
Pia
Hanscana amesema kwamba yeye na Khalfani ni marafiki japo hawajawahi
kufungua kampuni moja ila wakati wanatafuta maisha waliwahi kuishi
nyumba moja kwa sasa kinacho watenganisha ni kutokana na kila mmoja
kuzidi kutafuta maisha yake japo bado ni marafiki.
0 comments:
Post a Comment