![]() |
| RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE PAMOJA NA MAOFISA WA NBA WAKISHUHUDI MCHEZO WA FAINAILI |
RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa nchi ya
Tanzania itang’ara katika michezo kama kuna hamasa zitaendelea
Dkt Kikwete lisema hayo wakati wa mchezo fainali ya ligi ya
mpira wa kikapu ya Junior NBA uliofanyika katika kiwanja cha Jakaya Mrisho
Kikwete Park jiji Dar es Salaam,
Ligi hiyo ilishindanisha shule 30 za sekondari zilizo jijini
yaliyodumu kwa miezi tisa ambapo katika fainali hiyo iliwakutanisha timu ya
Lord Baden iliyoshinda mabao 22-18 dhidi ya Tusiime kumbukumbu 22-18
Amesema moja ya dalili njema ni uwanja huo unarekodi ya
vijina 50,000 wanaohudhuria katika mafunzo ya michezo
mbalimbali anahudhuria mafunzo katika michezo mbalimbali
Alisema kuwa kutokana na mafunzo hayo baada ya miaka mitanon
au 10 vijana watatoka vijana wazuri katika michezo.
Amesema kuwa tayari vijana wawili wamechaguliwa kujiunga
katika timu ya taifa ambapo taifa hili baada ya miaka 10 litakuwa katika orodha
ya mataifa yanayofanya vizuri katika michezo.
Dkt Kikwete alitoa wito kwa vilabu vya soka kuanzisha
mafunzo maalumu kwa ajili ya vijana ili kuimarisha kujenga timu yenye ufanisi
mkubwa utakao wasaidi kushindana katika mashindano ya kimataifa.

0 comments:
Post a Comment