KATIKA mahojiano yake ya kwanza tangu aingie ikulu
ya marekani Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliyekuwa akipinga Bima ya
afya ya Obama inayofaahamika kama Obama care, sasa amesema atafanyia
marekebisho machache kipengee cha sheria juu ya bima hiyo ya matibabu kwa
gharama nafuu.
Trump ametangaza
mageuzi makubwa ya sera punde atakapochukua nafasi ya Barack Obama katika Ikulu
ya White House mwezi Januari mwaka ujao.
Trump, aliyesisitiza
vikali kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa mamilioni ya Wamarekani
maskini kupata huduma ya afya kwa bei nafuu punde tu atakapochaguliwa rais,
yaonekana amebadilisha msimamo wake juu ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana
kulegeza msimamo wake juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule
amesema,Clinton ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa.

0 comments:
Post a Comment