| NAPE MNAUYE AKIMKABIDHI BENDERA MWAKILISHI WA TANZANIA KWENYE SHINDANO LA MISS AFRIKA JULITHA KABETE |
MWAKILISHI
wa Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika, Julitha Kabete ameondoka leo
kuelekea nchini Nigeria katika fainali ya michuano hiyo inayofanyika Novemba 26
mwaka huu huku akiwaahidi watanzania kua ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Akizungumza
kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kabete
amesema kuwa lengo lake ni kuwa mmoja wa wawakilishi bora katika shindano hilo
na kuitangaza vyema nchini pamoja na kurudi taji hilo na kwa.
kupitia kampuni
ya Millen Magese Group chini ya Mkurugenzi wake ,Happiness 'Millen' Magese
ameshukuru kwa kuingia nae mkataba ili aweze kushiriki michuano hiyo na kufanya
Kazi nyingine za urembo.
"Mimi
kama mwakilishi wa Tanzania nitahalikisha anafanya vizuri katika shindano hilo,
ambalo nimepata nafasi ya kuwa mpeperusha bendera wa nchini yangu Tanzania
" amesema.
Kabete
alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo,
Nape Nnauye ambaye alimshihi kwenda kujituma zaidi kwani wana imani na uwezo
wake na pia ni moja ya warembo watakaowakilisha vyema nchi yetu na kurudi na
taji hilo.
Lengo la
Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa
nyingine si tu akishapatikana mshinda wengine wanaachwa, hivyo tunaamini mrembo
huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri.
Shindano
hilo litafanyika nchini humo katika jimbo la Cross River, mji wa Calabar,ambapo
Gavana wa jimbo hilo la Cross River Profesa Ben Ayade, atatoa zawadi ya gari na
zaidi ya sh.million 52 ya Tanzania hiyo itakuwa kwa ushindi wa kwanza, mshindi
wa pili atapata zawadi ya Sh.milioni 32 na ushindi wa Tatu ni Sh.million 22.
Shindano
hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli mbiu ya Kutunza, Kujali
na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili
ya Maendeleo endelevu.
Julietha
alichaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG),
inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo pamoja.
Mmratibu wa
MMG, Matukio Chuma, amesema kuwa wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo
wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week.
Taasisi hiyo
imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini
Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani
na nje ya Bara la Afrika.
0 comments:
Post a Comment