KIPENGA cha kuashiria pambano limeanza kimeshapulizwa nchi
Marekani , ambapo leo sandukula kupiga kura litatoa maamuzi ya nani atakuwa
mrithi wa Rais Barack Obama kati ya Hillary Clinton na Donald Trump,anaandika Faki
Sosi.
Wagombea wote wawili hakuna ambaye unaweza kumtabiria zaidi
ya kusubiri kura za Wamarekani kuuamua nani awe Rais wao.
Ingawa mchungaji maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua
amemtabiri Clinton kushinda uchaguzi huo.
Kampeni zilipamba moto , vitisho , vijembe vilitawala
majukwaani katika kampeni za wagombea hao wawili lakini hadi kufikia leo hakuna
jambo baya lilijitokeza nchini humo.
BLOG YA WANANCHI itakujuza matokeo ya uchaguzi huo.

0 comments:
Post a Comment