November
4, 2016 U Heard ya XXL Clouds FM inayo sauti inayodaiwa ni ya Mama
mzazi wa mwigizaji Wema Sepetu akilalamika kuhusu marafiki wa Wema
kumtumia kwaajili ya kujinufaisha wao kibiashara kwa kumuuza kwa
wanaume.
Mama Wema
anasikika akisema kuna Rafiki wa mwanae anaitwa Muna alichukua nguo ya
ndani ya Wema ili aipeleke kwa waganga kwaajili ya kuchukua nyota yake
ambapo Wema alipotafutwa na Soudy Brown amejibu hana tatizo na Muna.
“Jamani
hakuna kitu kama hicho, mi niko poa na Muna… Hebu niacheni jamani nina
usingizi bwana, ila dah hilo jina la Muna (Ma****) kama limekick hivi
haki ya Mungu daaah! Binadamu sio watu wa mchezo aisee: – Wema Sepetu
Hivi
karibuni zilisambaa sauti zinazodaiwa ni za mama Wema zikisema kwamba
marafiki wa Wema wanamtumia kibiashara huku Wema akilalamika kuwa Muna
amekuwa amkimpa taarifa za uongo mama Wema ili aonekane mbaya.
“Yaani
kwakweli Wema hatofika popote kuna wale marafiki zake ni wachonganishi
wengine ni watu wazima sababu wengi wanamtumia kumuuza kwa wanaume na
wakimkosa wanaanza kutunga mambo ambayo sio, na Wema anaweza kuambiwa
kuna mtu anakuja kukuchoma mkuki, hata akiambiwa mama yako anakuroga
anaweza kuja mbio na anayabeba kama yalivyo’ – Mama Wema Sepetu
0 comments:
Post a Comment