![]() |
Na Sosy
SAMUEL Sitta ( 74) na Joseph Mungai ( 73) uswahiba wao ilianza tangu shule ya
sekondari ya Tabora Boys. Maswahiba hawa waliopishana mwaka mmoja tu moja na watazikwa siku moja wanahistoria yenye kufanana.
Wawili hao wamefariki ndani ya juma moja (wiki ) na kupishana siku moja tu.
Historia
ya maswahiba hawa ni wawili ambao wote upande wa mama zao wametokea
kwenye koo kubwa za mafichu hapa nchini.
Mama wa
marehemu Sitta, Zuena Said Fundikira, ni biinti wa Chifu Fundikira ambaye babu
yake ni Mtemi Isike Kiyungi.
Mama wa marehemu Mungai anatokana na ukoo wa Malangalila
unatokana na Chifu Mkwawa. Hivyo akina Malangalila na Mwamuyinga ni wajomba
zake Joseph Mungai kutoka ukoo wa Kichifu wa Mkwawa.
Wawili hawa mbali ya uswahiba wao wa
tangu shule uliowapelekea hadi kufanya kazi kama Mawaziri kwenye Serikali ya
Awamu Nne.
Ni
watani wa jadi. Kwa vile Wahehe chini ya Chifu Mkwawa walipigana na
Wanyamwezi chini ya Mtemi Isike .
Katika namna ya kusuluhisha mgogoro,
Chifu Isike alimuozesha binti yake kwa Chifu Mkwawa. Kikosi kidogo cha
Wakonongo kilitumwa na Isike kumsindikiza binti huyo. Walipoikaribia Iringa,
Mkwawa alituma watu wake kwenda kumpokea binti huyo nje kidogo ya Iringa mahali
ambapo hadi hii leo panaitwa Ikonongo.
Na Wakonongo wale waliamua kuweka
makazi yao hapo. Ni nje kidogo ya Manispaa ya Iringa, na dalili za ujio wa
Wakonongo hapo ni uwepo , hadi leo, wa watu wa asili ya Kikonongo na miti mingi
ya miembe waliokuja nao Wakonongo kutoka Tabora, enzi hizo.
Ni simanzi kwa maswahiba hawa kutuagana
Chifu Mungai ameagwa leo, na mwenzake Chifu Sitta ataagwa kesho. Wote wawili
watazikwa katika siku moja ya Jumamosi, mmoja Mufindi na mwingine Urambo.

0 comments:
Post a Comment