Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza
betri moyoni katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), amefariki
dunia.
Mama
mzazi wa Happiness, Elitruda Malley amesema Happiness alifariki dunia ghafla
juzi mchana.
Alisema
Jumapili, mtoto huyo alikuwa mzima na walikwenda kanisani kutoa sadaka ya
shukrani kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyowatendea na wakarudi
nyumbani salama.
“Jana
tumeamka vizuri lakini ghafla hali yake ilibadilika akaanza kulalamika kuwa
anajisikia vibaya, tukamkimbizia Hospitali ya Selian hapa Arusha lakini tukiwa
njiani alifariki dunia,” alisema.
Elitruda
alisema kifo cha mwanawe kimemhuzunisha mno na daima atamkumbuka.
“Alikuwa
tayari amesharudi shuleni, alikuwa akiniambia kuwa atasoma kwa bidii ili ndoto
yake ya kuwa daktari bingwa itimie aweze kusaidia watu wanaosumbuliwa na
magonjwa mbalimbali,” alisema.
Hata
hivyo, alisema maziko ya Happiness yanatarajiwa kufanyika leo huko Mbulu mkoani
Manyara.
Mkurugenzi
wa JKCI, ambako Happiness alifanyiwa upasuaji, Profesa Mohamed Janabi amesema
taarifa hiyo imemshtua ikizingatiwa mtoto huyo alikuwa anaendelea vizuri.
“Sikuwa
na taarifa, nitawasiliana na mama yake tujue hasa shida gani ilitokea, maana
zipo sababu nyingi labda alipita jirani na mitambo ya umeme au simu, hizo ni
sehemu hatarishi kwa mtu aliyewekewa betri kwenye moyo,” alisema.
Happiness
alifanyiwa upasuaji huo wa historia nchini Julai 15, mwaka huu katika Taasisi
ya JKCI wa kuwekewa betri maalumu kwenye moyo ambayo kitaalamu inaitwa
‘pacemaker’.
Kwa
mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibia mtoto huyo, wakati alipopekekwa
hospitalini hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa 20.
Walisema
hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwa vile anapaswa kuwa na wastani wa mapigo
60 hadi 100 kwa umri wake.
Mtoto
Happiness alizaliwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi hali hiyo huwakumba watu
wazima.
Moja
ya ndoto za mtoto huyo ambayo alinukuliwa akiisema ni kuwa daktari bingwa wa
kutibu magonjwa mbalimbali.GPL(P.T)

0 comments:
Post a Comment